Ligi kuu ya FKF huenda ikachelewa kuanza alia Rais wa FKF

Msimu mpya wa ligi kuu ya FKF mwaka 2020/2021 huenda usianze Ijumaa ya Novemba 20  ilivyoratibiwa.

Kulingana na kinara wa shiriksho la kandanda Kenya Nick Mwendwa , Wizara ya michezo haijaidhinisha ratiba na ombi walilopokea kutoka kwao kuhusu kuruhusu kuanza kwa ligi hiyo.

“Kwa sasa tunahofia huenda ligi ikakosa kuanza tulivyopanga Novemba 20 ,kwa sababu wizara haijatujibu,lakini hata hivyo bado tuwaandikia barua nyingine tuone kama wataturuhusu kuanza ligi vile tumepanga’’akasema Mwendwa

Mwendwa alielezea masikitiko yake kuwa endapo ligi itakosa kuanza huenda wachezaji wengi wakataabika kwa kukosa pesa ambapo zinapaswa kutolewa na wafadhili na pia huenda hata wafadhili hao wakajiondoa.

“Ingekuwa bora ligi ianze,nahofia kama haitaanza wachezaji watajosa pesa kutoka kwa sponsers ambao wanatakiwa kutoa pesa baada ya kaunza kwa ligi na pia huenda hao sponsers wakajiondoa’’akaongeza Mwendwa

Msimu mpya wa ligi uliratibiwa kuanza Novemba 20 na kukamilika Mei mwakani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *