Lewandowski avunja ukiritimba wa Ronaldo na Messi na kushinda tuzo ya FIFA ya mwanasoka bora
Mshambulizi wa Poland na klabu ya Bayern Munich Rober Lewandowski alitawazwa mwanasoka bora wa mwaka katika tuzo za Fifa Alhamisi usiku.
Lewendowksi aliye na umri wa miaka 32 aliongoza Bayern Munich kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Ulaya kando na kushinda ligi kuu Ujerumani na kombe la Ujerumani na kuibuka mfungaji bora nchini ujerumani na katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Mshambulizi huyo wa Poland ndiye mwanasoka wa kwanza kuvunja utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionell Messi katika tuzo za FIFA tangu Ronadhino Gauto mwaka 2005 ni kwa mwaka wa pili ndani ya miaka mitano ambapo Ronaldo na Messi wanapigwa kumbo katika tuzo hiyo.
Orodha ya mwisho ya tatu bora ilikuwa na Lewandowski Roaldo na Messi huku mshambulizi huyo wa Poland akiwa mchezaji wa kwanza anayepiga soka ya kulipwa nchini Ujerumani kunyakua tuzo huyo.
Lewandowski alipata kura 52 akifuatwa na Ronaldo kwa kura 38 ,tatu zaidi ya Messi.
Kwa Jumla Ronaldo amenyakua tuzo hiyo ya FIFA mara mbili mwaka 2016,2017 ,Messi akainyakua mwaka 2019 naye Luka Modric akitawazwa mshindi mwaka 2018.
Tuzo ya mchezaji bora kwa wanawake ilinyakuliwa na beki wa Uingereza Lucky Bronze baada ya kuwapiku Wendie Renard wa Ufaransa na Parnille Hander wa Norway.
Jurgen Klopp aliibuka kocha bora wa mwaka kwa wanaume kwa mwaka wa pili mtawalia kwa kuiongoza the reds kushinda taji ya ligi kuu Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 30 na kuzoa alama 99 .
Klopp aliwashinda Marcelo Bielsa wa Leeds United na Hans Dieter Flick wa Bayern Munich.
Sarina Wiegman wa Uholanzi alinyakua tuzo ya kocha bora wa mwaka kwa wanawake .