Leopards yamnasa kiungo wa Congo

Miamba wa soka nchini Kenya Afc Leopards wamekamilisha usajili wa kiungo wa kutoka nchini Congo Fabrice Mugheni  kutoka kilabu ya  Rwanda Rayon Sports inayoshiriki ligi kuu ya Rwanda .

Mwanadinga huyo ambaye zamani alizichezea timu za Police FC na Kiyovu sports club anajiunga na Ingwe kwa kandarasi ya miaka miwili .

Leopards wamepiga kambi ya mazoezi ya nyanda za juu huko Iten kujiandaa kwa msimu mpya.

Ingwe wanyakua taji ya ligi kuu nchini Kenya mara 12 huku wakisubiri zaidi ya miaka 22 tangu watwae kombe hilo .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *