Leopards wanoa kucha kwa kumsajili chipukizi Bienvenue

Vigogo wa soka humu nchini wameongeza makali yao wanapojiandaa kwa msimu mpya wa ligi baada ya kumsajili mshambulizi Bienvenue Shaka kutoka kilabu ya  Tunisia  Etoile Sportif du Sahel.

Chipukizi huyo aliye na umri wa miaka 20 kutoka Burundi aliandikisha mkataba na Leopards maarufu kama Ingwe ,baada ya kuwachezea miamba wa Tunisia Etoile Du Sahel katika ligi kuu kwa miaka miwili .

Awali Bienvenue aliichezea kilabu ya Burundi ya Aigle Noir ,timu za taifa za Burundi kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 na miaka 23 kabla ya kujumuishwa katika timu ya taifa Intamba Murugamba.

“Nafurahia kujiunga na Afc Leopards , klabu kubwa nchini  Kenya. Nitashirkiana na wenzangu kwenye timu ili kuleta ufanisi na pia naomba support kutoka kwa mashabiki”  akasema Shaka

Shaka tayari amejiunga na kikosi cha Ingwe kilicho katika kambi ya mazoezi ya nyanda za juu mkoani bonde la ufa.

Leopards pia imenasa sahihi ya kipa John Oyemba kutoka Kariobangi Sharks kwa kandarasi ya miaka miwili .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *