Kpl yapoteza kesi dhidi ya Fkf

Shirikisho la kandanda nchini Fkf limeshinda kesi iliyowasilishwa na kampuni ya KPL .

Kampuni ya Kpl iliwasilisha kesi katika mahakama ya kutatua migogoro ya michezo nchini SDT kupinga uamuzi wa Fkf kutamatisha msimu wa mwaka 2019,2020 wa Kpl huku ikiwatawaza Gor mahia Mabingwa  kutokana na janga la Covid 19.

Katika uamuzi wa leo uliodumua dakika 30 kupitia zoom ,mwenyekiti wa Mahakama  hiyo, John Ohaga amesema hatua ya fkf kumaliza msimu na kuwapa Gor Mahia ubingwa haikuwa na dosari kwani ugonjwa wa covid 19 lilikuwa janga la kitaifa.

Ohaga amesema kuwa Kpl haikutumia njia zote zilizostahili kabla ya kuishitaki fkf , na Pia Ceo wa Kpl Jack Oguda aliwasilisha kesi hiyo kibinafsi bila kushirikisha vilabu katika ligi hiyo.

Ohaga  pia amemtaja kinara wa  FKF  Nick Mwendwa alifanya kosa kutangaza kukamilishwa kwa msimu wa ligi kwani hakuwa na mamlaka kisheria kufanya hivyo ,kutokana na kutokuwepo kwa baraza kuu Nec ambalo muda wake wa kuhudumu ulikuwa umemalizika mwezi Februari.

Jaji Ohaga pia ametupilia mbali ombi la Oguda la kutaka alipwe ridhaa iliyoletwa na hasara ya kumaliza msimu kwa ghafla.

Uamuzi wa leo unaonekana kuzima tofauti na vuta ni kuvute ya muda mrefu ambayo imekuwepo baina ya Kpl na Fkf kwa takriban miaka minne iliyopita.

Kufuatia uamuzi wa leo pia Gor Mahia ambao ni mabingwa wa ligi wako huru kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika na kujiandaa kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu utakaoendeshwa na Fkf.

Fkf pia itaendelea mbele na uchaguzi wa kaunti utakaondaliwa jumamosi hii ,ukifuatwa na ule wa kitaifa tarehe 17 mwezi ujao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *