Korona: Watu 152 waambukizwa, wagonjwa 39 wapona na wengine 3 wafariki

Kenya imenakili visa vipya 152 vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,213 zilizopimwa katika muda was aa 24 zilizopita.

Visa hivyo vipya vimetokana na sampuli za Wakenya 144 na 8 za raia wa kigeni ambapo 83 ni wanaume na 69 ni wanawake, kati ya umri wa miaka saba hadi 79.

Jumla ya visa vilivyothibitishwa humu nchini vimetimia 106,125 na vimetokana na upimaji wa jumla ya sampuli 1,301,051.

Visa hivyo vimenakiliwa katika magatuzi mbali mbali kama ifuatavyo: Nairobi 131, Kiambu 10, Machakos 4, Kajiado 2, Nyeri 2, Meru 1, Mombasa 1 na Murang’a 1.

Wagonjwa 39 waliokuwa wakiugua maradhi ya korona wamepona kikamilifu, 23 walikuwa wakitibiwa nyumbani na 16 wakaruhusiwa kuondoka kutoka vituo vya afya na kufikisha jumla ya wagonjwa waliopona hadi 86,717.

Idadi ya watu waliofariki imefikia 1,859 baada ya wagonjwa watatu zaidi kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Kwa sasa wagonjwa 1,527 wanashughulikiwa nyumbani huku 357 wakiwa wamelazwa hospitalini ambapo 57 wako katika kitengo cha wagonjwa mahututi, 25 wakiwa kwenye vifaa vya kusaidia kupumua na 28 wakipokea hewa ya ziada ya oksijeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *