Kocha wa Togo Claude Le Roy ang’atuka baada ya kuwa usukani kwa miaka mitano

Kocha wa Togo Claude Le Roy amejiuzulu baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka mitano huku akishindwa  kuifuzisha kwa fainali za mwaka ujao za kombe la AFCON.

Mfaransa huyo aliye na umri wa miaka 73 alishika hatamu za kuinoa Togo maarufu kama the Hawks mwaka 2016 huku akiwafuzisha kwa fainali za AFCON mwaka 2017 nchini Gabon lakini ikashindwa kufuzu mwaka 2019 na pia mwaka ujao nchini Cameroon.

Claude Le roy

Kwa Jumla Le Roy ameiongoza Togo kwa mechi 35 za kimataifa akishinda 9 kutoka sare 12 na kupoteza 14, hivi punde  ikiwa kichapo cha nyumbani dhidi ya Kenya katika mchuano wa kufuzu kwa fainali za mwakani za AFCON.

Le Roy amejiuzulu kwa maafikiano na shirikisho la soka nchini Togo FTF na waziri wa michezo Dkt Bessi Lidi Kama na sasa wataanza sakasaka za mkufunzi mpya kabla ya mechi za kufuzu kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar mechi zitakazoanza Juni mwaka huu ,Togo ikijumuishwa kundi  H pamoja na Senegal,Congo na Namibia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *