Categories
Michezo

Kocha wa Italia Mancini augua COVID 19

Kocha wa Italia Roberto Mancini amepatikana na ugonjwa wa Covid 19 .

Imebidi kocha huyo aliye na umri wa miaka 55  ambaye pia  amewahi kuwa mkufunzi wa Manchester City kutoka mwaka 2009 hadi 2013 ajitenge nyumbani kwake Rome huku akisema kuwa hana dalili zozote za ugonjwa huo.

Italia maarufu kama the Azzuri  wamepangiwa  kucheza mechi tatu ndani ya majuma mawili yajayo , ikiwemo moja ya kirafiki dhidi ya Estonia Jumatano ijayo na mechi mbili za kombe la ligi ya mataifa ya ulaya dhidi ya  Poland na Bosnia .

Mwitaliano huyo awali aliifunza Inter Milan iliponyakua mataji matatu mtawalia ya Serie A  kabla ya kujiunga na Mancity alipotwaa ligi kuu Uingereza mwaka 2012 na kombe la FA mwaka 2011 na alishika hatamu za kuifunza Italia baada ya kukosa kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 aliposhinda mechi 10 za kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2020.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *