Kocha Musa ana imani ya Kenya kufuzisha mabondia wengi Olimpiki

Kocha mkuu wa timu ya Kenya ya ndondi  Musa Benjamin ana imani kuwa atakwua na kikosi kikubwa na dhabiti kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka huu.

Musa amesema haya alipoongoza mazoezi ya timu hiyo mtaani Lavington akiongeza kuwa kufikia sasa mazoezi yamekuwa mazuri na lengo lake sio kufuzisha tu mabondia kwa michezo ya Olimpiki bali pia kunyakua nishani.

“Mambo  tunayoyashughulikia kwa sasa ni Cardiovascular training,muscle training na strength and conditioning,wachezaji wanarespond vizuri pia kuna improvement katika punching,movement into range na out of range pamoja na counter punching skills .tunataka tukuwe katika nafasi nzuri ya kuwafuzisha wachezaji wengi na kushinda medali Olimpiki”akasema Musa

Kocha Musa ameitaka serikali na kamati ya Olimpiki nchini Nock kuandaa mapigano ya kujipima nguvu kw atimu hiyo kabla ya mashindano ya kufuzu kwa olimpiki mwezi Juni mjini Paris Ufaransa na michezo hiyo ya Olimpiki mwezi Julai.

“Tunaiomba serikali na Nock kuwezesha timu kuwa na mapigano kadhaa ya kujipima nguvu kabla ya mashindano ya kufuzu nchini Ufaransa mwezi Juni  na michezo ya Olimpiki ya mwezi Agosti ili timu iwe katika hali nzuri “akaongeza kocha Musa

Hadi sasa mabondia wawili wamejikatia tiketi kwa michezo hiyo ya Olimpiki na upo uwezekano wa kupitisha idadai ya mabondia 3 walisohiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *