Categories
Michezo

Kocha mpya wa Gor Mahia Vaz Pinto asaini mkataba wa miaka miwili

Kocha mpya wa Gor Mahia Carlos Vaz Pinto amesema lengo lake ni kuhakikisha Gor Mahia wanafuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho mwaka huu.

Pinto ambaye ni rai wa Ureno ,amesema haya mapema Jumapili baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na Kogalo akisisitiza kuwa tajriba pana aliyo nayo kufanya kazi ya ukunzi barani Afrika itamsaidia pakubwa katika majukumu yake mapya.

“Lengo langu kuu ni kuifuzisha Gor Mahia kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho pamoja na kushinda mechi katika ligi na kuandikisha historia,tuna muda wa kutosha kuwasoma wapinzani wetu NAPSA na pia timu yangu ili kuleta matokeo” ‘akasema Pinto

Mreno huyo ameongeza kuwa atalenga kushinda mataji akiwa na Gor  kwa kuwa ni klabu kubwa .

“Nimefurahia kujiunga na Gor Mahia ambayo ni timu kubwa na nimekuja kuandikisha historia”akaongeza Pinto

Kwa upande wake mwenyekiti wa Gor Ambrose Rachier amesema wamelazimika kumtafuta kocha mpya baada ya kutamatisha kandarasi ya Robertinho kwa maafikiano.

“Imebidi tumtafute kocha mpya miezi minne tangu tumzindue kocha Oliveira kutoka Brazil kuiongoza Gor baada ya Caf kurekebisha vikwazo vya cheti cha kufuzu ili kusimamia mechi za bara Afrika,imekuwa vigumu kumsubiri kocha Oliveira kwa miezi minne ijayo ili aendelee na kazi yake baada ya kwenda kuongeza masomo, na ndio tumeafikiana naye tukatize kandarasi yake na tutafute kocha mpya”akasema Rachier

“Tunamshukuru Pinto kwa kukubali ombi letu na inavyoonekana tunahitaji kuimarisha idara yetu ya tiba maungo ndio maana pia tumemzindua kocha Khamis Juma Musa kuwa physiotherapist wetu,tuna imani ujio wa wawili hawa kutaongeza makali kwenye timu huku pia tukiendelea kumtafuta kocha msaidizi”akaongeza Rachier

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *