Kitaeleweka Gor dhidi ya APR Nyayo

Mabingwa wa Kenya Gor  Mahia watashuka uwanjani Nyayo Jumamosi saa kumi alasiri  kupambana na  APR kutoka Rwanda katika marudio ya mchujo wa ligi ya mabingwa Afrika  CAF .

Gor watacheza mchuano huo bila mashabiki katika uwanja wa Nyayo huku wakihitaji ushindi wa bao 1-0 ili kuingia awamu ya pili ya mchujo baada ya kuambulia kichapo cha magoli 2-1 wiki jana katika duru ya kwanza mjini Kigali.

Wasimamizi wa Gor wamerekebisha makosa yaliyotokea katika mkondo wa kwanza huku wakilenga kucheza hadi hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.

Mshindi wa mechi ya leo kwa jumla atakuchuana na aidha Al Nasr ya Libya au Cr Belouzidad ya Algeria katika mchujo wa pili .

Pambano hilo litarushwa mbashara na runinga ya KBC Channel one .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *