Kisumu All Stars yanusia kusalia ligini msimu ujao

Timu ya Kisumu All Stars imeweka hai matumaini ya kusalia katika ligi kuu msimu ujao,baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Vihiga United Fc katika mkondo wa kwanza wa mchujo wa kupiga ligi kuu  uliosakatwa Jumamosi alasiri katika uwanja wa Mumias Sports Complex.

Willis Otenda alipachika bao la kwanza kwa wageni Kisumu All Stars kupitia mkwaju wa penati baada ya difenda wa  Vihiga  Michael Odongo kumwangusha mshambulizi  Erick Otieno  bao hilo likidumu hadi mapumziko.

Vihiga walianza vyema  kipindi cha pili kwa mashambulizi tele yaliyozaa matunda baada  Dennis Wafula kuisawazishia kunako dakika ya 54.

Hata hivyo azma  ya wenyeji kupata ushindi yalididimizwa dakika moja baadae ,baada ya  Shadrack Omondi kufyatua tobwe kutoka umbali wa mita 20 na kuwapa All Stars bao la ushindi.

Timu hiyo ya kaunti ya Kisumu sasa itawaalika Vihiga Tarehe 4 mwezi ujao huku mshindi wa jumla akifuzu kuchezqa ligi kuu  wakati wa msimu mpya utakapoanza Novemba 20.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *