Kisumu All Stars kukabana koo na Vihiga United Jumamosi kuwania kushiriki ligi kuu ya Fkf

Timu za Vihiga United Fc na Kisumu All Stars zitapamabana Jumamosi  Alasiri katika uwanja wa Mumias Sports Complex katika mkondo wa kwanza

wa fainali ya kuwania kupandishwa daraja kucheza ligi kuu.

Vihiga iliibuka ya tatu katika ligi ya Supa nao All Stars wakamaliza katika nafasi ya 16 kwenye ligi kuu Kpl msimu uliopita .

 

Wachezaji    wa     Vihiga      United Fc

Marudio ya fainali hiyo kupigwa Novemba 4  katika uwanja wa Moi Kisumu, huku mshindi wa jumla akifuzu kupiga ligi kuu katika msimu mpya unaotarajiwa kuanza baadae mwezi ujao.

Wachezaji na maafisa wa timu hizo mbili walipitia vipimo vya Covid 19  kwa mjibu wa masharti ya wizara ya michezo na ile ya Afya.

All Stars ndiyo timu pekee ya kutoka kaunti ya Kisumu na eneo la Nyanza kwa jumla iliyokuwa ikishiriki ligi kuu msimu uliopita na watakuwa wakilenga kusalia ligini wakati Vihiga wakipambana kurejea katika ligi tangu washushwe ngazi kutoka ligi kuu Kpl  Mei mwaka uliopita .

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *