Kipute cha ligi ya mabingwa Ulaya kuanza Jumanne

Kindumbwendumbwe cha kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya kitaanza rasmi Jumanne usiku  Oktoba 20 kwa mechi za kwanza hatua ya makundi.

Timu nne mpya  zilifuzu kwa hatua hiyo makundi yenye timu 32 kwa mara ya kwanza nazo ni Basaksehir Uturuki, Krasnodar ya Urusi, Rennes ya Ufaransa na Midtjylland kutoka Denmark.

Bayern Munich wakipiga gwaride baada ya kutwaa ubingwa msimu jana

Kulingana na droo ya makundi  kutakuwa na mechi kadhaa za kusisimu ikiwemo pambano baina ya Juventus na Barcelona Oktoba 28 litakalowakutanisha Lionell Messi na Cristiano Ronaldo na mechi ya Jumatano Oktoba 21 ya kundi A mabingwa watetezi Bayern Munich yake Robert Lewandowski ikimenyana na Atletico Madrid ya Luis Suarez.

Mechi za pili za makundi zitachezwa baina ya Oktoba 27 na 28 ,mechi za tatu Novemba 3 na 4 na zile za nne Novemba 24 na 35.

Baadhi ya wachezaji wa Liverpool wakiwa mazoezini

Baadae kutakuwa na mechi za 5 za makundi kati ya Desemba mosi na mbili huku michuani ya makundi ikikamilika  Desemba  8 na 9 mwaka huu .

Awamu ya 16 bora itasakatwa baina ya februari 16 na 17 na Februari 23 na 24 huku marudio yakiwa Machi 9 na 10 na Machi 16 na 17 mwaka ujao kwa michuano ya marudio.

Kipute hicho  kitaingia robo fainali April 6 na 7 na April 13 na 14 mwaka ujao  ikifuatwa na semi fainali April 27 na 28 kwa mkondo wa kwanza  Mei 4 na 5 mwaka ujao na kisha fainali ichezwe katika uwanja wa Ataturk Olympic mjini Istanbul Uturuki.

Uwanja wa Atartuk nchini Uturuki utakaoandaa fainali

Katika baadhi ya mechi za ufunguzi Jumanne usiku Dynamo Kiev ya Ukraine watawaalika Juventus kutoka Italia,nao Barcelona wawaandae Farencvaros ya Hungary katiak kundi G .

Kwenye kundi H Manchester united wako ugenini kwa Psg ya ufaransa uagni Parc Des Princess nao Lazio kutoka Italia watawatumbuiza Borusia Dortmund ya Ujerumani nao mabingwa wa Europa league Sevilla watakwua wageni wa Chelsea katika kundi E.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *