Kipute cha CHAN kuandaliwa baina ya Januari na Februari 2021

Makala ya 6 ya kinyanganyiro cha kombe la mataifa ya Afrika kwa wanasoka wanaocheza ligi za nyumbani yataandaliwa kati ya Januari 16 na Febrauri 7 mwaka ujao nchini Cameroon.

Pambano la ufunguzi litakuwa baina ya wenyeji Cameroon dhidi ya Zimbabwe ,kabla ya Mali kupimana nguvu na Burkinafasso mechi zote zikiwa za kundi A.

Michuano ya kundi B kuanza Januari 17 ,Libya wakiwa na miadi dhidi ya Niger huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo ikicheza dhidi ya Congo Brazaville.

Moroko na Togo watakumbana katika pambano la kundi C januari 18 nao Uganda na Rwanda ,ilihali mechi za kundi D zitaanza Januri 19 kwa mchuano kati ya Namibia na Zambia huku Tanzania ikifunga kazi dhidi ya Guinea.

Ratiba kamili ya kipute cha Chan mwaka ujao nchini Cameroon

Mechi za kwota fainali ziktaandaliwa baina ya  Januauari 30 na 31  nazo nusu fainali zichezwe Februari 3,ikifuatwa na mechi wakati fainali ikisakatwa mjini Younde.

Mechi za kundi A zitaandaliwa mjini Younde,Kundi B mjini Japoma Doula ,kundi C reunification duala wakati kundi D likipiga kambi mjini Limbe.

Mataifa 16 yatawania kombe hilo linaloshikiliwa na  Moroko ndio mabingwa watetezi baada ya kutwaa kombe hilo miaka miwili iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *