Kimbunga Vamco chasababisha watu kutoroka makazi yao Vietnam

Kimbunga kikali kilichosababisha vifo vya watu kadhaa nchini ufilipino sasa kinaelekea Vietnam, na kuwafanya maelfu ya watu kutoroka makazi yao.

Kibunga hicho kwa jina Vamco kinatarajiwa kukumba eneo la mashariki ya Vietnam siku ya Jumaopili.

Viwanja vya ndege na fuo zimefungwa huku wavuvi wakitakiwa warejee kwenye nchi kavu huku nchi hiyo ikijiandaa kwa upepo mkali unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 100 kwa saa.

Kimbunga hicho kilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika kisiwa kikubwa zaidi nchini ufilipino cha Luzon.

Yamkini watu 42 waliaga dunia huku wengine 20 wakiwa hawajulikani waliko nchini ufilipino baada ya kimbunga Vamco kukumba nchi hiyo siku ya Jumatano juma moja pekee baada ya kimbunga kikali zaidi kuwahi kukumba nchi hiyo katika muda wa miaka saba cha Goni.

Nchini Vietnam, maelfu ya watu katika majimbo manne ya katikati ya nchi hiyo wamehamishwa kulingana na halamshauri ya kukabiliana na majanga.

Vimbunga kadhaa vimekumba nchi hiyo katika majuma ya hivi maajuzi huku zaidi ya watu 100 wakiaga dunia kufuatia mafuriko mwezi uliopita baada ya mvua kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *