Kimanzi arejea kwa mbwembwe ligi kuu akisaini mkataba wa miaka 4 na Wazito Fc

Aliyekuwa mkufunzi wa Harambee Stars Francis Kimanzi ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya  Wazito Fc inayoshiriki ligi kuu  kwa mkataba wa miaka minne .

Uteuzi wa Kimanzi unajiri takriban wiki nne tangu afurushwe kuwa kocha mkuu wa  timu ya taifa Harambee Stars .

Kimanzi ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Mathare United atasaidiwa na kocha wa zamani wa Thika United John Kamau katika majukumu mapya huku wakiwa huru kuwatafuta wasaidizi wao.

Wazito Fc hawajakuwa na kocha tangu wampige kalamu  Fred Ambani na msaidizi wake Salim Babu tarehe 9 mwezi huu .

Kimanzi ni kocha wa 7 kujiunga na Wazito Fc katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita baada ya Ambani,Mwingereza  Stewart Hall, Stanley Okumbi, Fred Ouna, Hamisi Abdalla na  Melis Medo.

Uzinduzi rasmi wa Kimanzi na msaidizi wake utaandaliwa Jumatano katika makao makuu ya kilabu hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *