Kim Kardashian aongoza watu wengine mashuhuri Marekani kususia instagram

Mwanamke maarufu nchini marekani Kim Kardashian hii leo anaongoza watu wengine mashuhuri nchini humo katika kususia mtandao wa Instagram.

 

Watu hao mashuhuri wanafanya hivyo kama njia moja ya kuonyesha kutoridhishwa na kampuni ya mitandao ya kijamii kwa jina Facebook ambayo wanasema imeshindwa kudhibiti maneno ya kusababisha chuki na habari za uongo kwenye mitandao yao.

 

Kampuni kubwa kubwa ambazo hufanya matangazo ya mauzo kwa wingi pia zilifanya kususia mitandao ya kijamii chini ya kauli mbiu “stop hate for profit” mwezi Julai. Kampuni hizo ni kama vile Starbucks, Cocacola na Verizon.

Kundi hilo la watu mashuhuri likiongozwa na Kim Kardashian linataka Facebook iondoe makundi yaliyo kwenye facebook ambayo yanasemekana kuendeleza ubaguzi wa rangi, chuki na mipango ya vurugu.

Mfano mwema ni kisa ambapo Facebook ilikataa kuondoa kundi la waasi la eneo la Kenosha huko Winscosin nchini Marekani hata baada ya raia wengi wa marekani kutuma maombi ya kuondolewa kwa kundi hilo kwenye Facebook.

Watu maarufu ambao wako kwenye mpango wa leo wa kususia Instagram ni kama vile Sacha Baron Cohen, Naomi Campbell, Judd Apatow, Amy Schumer, Sarah Silverman, Kate Hudson, Leonardo DiCaprio, Rosario Dawson, Isla Fisher, Scooter Braun na Mark Ruffalo.

Kim Kardashian West ni mmoja wa watumizi wa Instagram walio na wafuasi wengi zaidi.

 

Kampuni ya Facebook haijasema lolote kuhusu swala hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *