Kevin De Bryune kusalia Etihad hadi mwaka 2025

Kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne amesaini mkataba mpya na mabingwa hao watarajiwa wa ligi kuu Uingereza hadi mwaka 2025.

Mbelgiji huyo aliye na umri wa miaka 29 alikuwa amesalia na miaka miwili kwenye kandarasi yake  ya awali,akijivunia kushinda mataji mawili ya ligi kuu Uingereza ,kombe la FA,na League cup mara nne tangu atue Manchester  kutoka Wolfsburg mwaka  2015.

Licha ya kusumbuliwa na msururu wa majeraha, De Bruyne amepachika kimiani magoli 8 na kuchangia mengine 33 katika mechi 33 alizocheza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *