Kesi zitawasilishwa mahakamani kwa mfumo wa dijitali

Idara ya mahakama inazindua mfumo wa dijitali wa kuwasilisha kesi zote huku ikiondoka kutoka kwa mfumo wa kawaida wa kuwasilisha kesi ambao unaweza kutumiwa vibaya.

Akiongea wakati wa wiki ya uhamasisho wa kisheria wa chama cha wanasheria nchini-LSK, kaimu naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma anayehusika na idara inayoshughulikia hatia, Jacinta Nyamosi, alisema ili kuimarisha huduma za kufungulia watu mashtaka ipo haja kwa kesi  zote kuwasilishwa mtandaoni ili ziweze kufuatiliwa kwa urahisi.

Akiongea wakati wa wiki ya uhamasisho, Nyamosi alisema huduma sawa na hizo zitasambzwa hadi kaunti nyingine kufikia mwisho wa mwaka huu.

Nyamosi alisema hatua hiyo ni ya kujitolea kuimarisha utoaji huduma za kitaalam za kufungulia watu mashtaka.

Naibu msajili wa idara ya mahakama, Elizabeth Tanui, alisema mara mfumo huo utakapoanza kutumika hakutakuwa na haja kwa Wakenya kwenda hadi ofisi ya msajili wa mahakama kuwasilisha kesi zao.

Tanui alisema idara ya mahakama inazingatia teknolojia mpya ya kuharakisha uwasilishaji kesi.

Mwanachama wa chama cha wanasheria nchini, Aileen Aluso Ingati, alihimiza serikali kutoa nafasi sawa kwa raia wote akisema teknolojia haipaswi kutumiwa kuwabagua wasiojimudu katika jamii.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *