Kenya yaungana na mataifa ya Afrika kwenye azimio la utunzi wa mazingira

Kenya imeidhinisha rasimu ya azimio la mawaziri wa Barani Afrika linalosisitiza kujitolea kwa mataifa ya Afrika katika kulinda mazingira yake na maliasili licha ya changamoto na matatizo yanayokana na janga la maradhi ya COVID-19.

Waziri wa Mazingira na Misitu Keriako Tobiko amesema nchi hii inaunga mkono maoni ya viongozi wa ulimwengu pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres na  Mawaziri wa  Mazingira na Fedha barani.

Wadau hao wanasisitiza haja ya hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na maendeleo endelevu na  kuwekwa kwa  mikakati ya kutunza mazingira baada ya  kuisha kwa janga la maradhi ya COVID-19.

Tobiko pia alitangaza  kuwa  nchi hii inatambua maazimio ya Muungano wa Afrika kuhusu utunzi wa Mazingira kama msingi wa ustawi wa uchumi wa jamii na kuwepo kwa fedha za kutosha kukabiliana na mabadiliko hali ya hewa kwa ajili ya kufanikisha kuafikiwa kwa ruwaza muungano huo ya mwaka wa 2063.

Alisema pia kupitia kuanzishwa kwa hazina ya kitaifa ya kukabiliana na maradhi ya COVID-19 na kitita cha Shilingi bilioni 54 kutoka kwa serikali, huku bilioni 2 zikilengwa kutumika kwa hatua za utunzi wa misitu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Serikali ina mpango wa kuanzisha hazina ya misitu ili kusaidia sekta ya kibinafsi kushiriki katika shughuli za misitu ya kibiashara ambazo zitatoa fursa ya ajira kwa vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *