Kenya yaripoti visa 85 vipya vya maambukizi ya COVID-19

Wizara ya Afya humu nchini imetangaza visa vipya 85 vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, kutokana na sampuli 2,985 zilizopimwa masaa 24 yaliyopita.

Visa hivyo vimeongeza idadi ya maambukizi hadi kufikia 99,983 kutokana na jumla ya sampuli 1,156,106 zilizopimwa kufikia sasa.

Visa 69 ni vya Wakenya huku 16 vikiwa vya raia wa kigeni, wanaume 46 na wanawake 39, wote wa kati ya umri wa mwaka mmoja hadi miaka 88.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 70, Kiambu 2, Makueni 2, Mombasa 2, Nyeri 2, Nakuru 2, Laikipia 1, Machakos 1, Narok 1, Nyandarua 1 na Trans Nzoia 1.

Wizara ya Afya pia imethibitisha kupona kwa wagonjwa 33 na kuifanya idadi jumla ya waliopona humu nchini kufikia 82,969.

Kati ya hao waliopona, 25 walikuwa wakitibiwa nyumbani ilhali wanane walikuwa wakitibiwa hospitalini.

Hata hivyo wagonjwa wanne zaidi wamethibitishwa kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha jumla ya maafa hadi 1,744.

Kufikia sasa, kuna jumla ya wagonjwa 545 wanaohudumiwa katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini huku wengine 1,568 wakiwa katika mpango wa uangalizi wa nyumbani.

Wagonjwa 27 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 15 kati yao wakitumia vipumuzi ilhali 11 wanapokea hewa ya oksijeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *