kenya yanakili visa 673 vipya vya Covid-19 huku watu 325 wakipona

Taifa hili Ijumaa limenakili visa  673 vipya vya Covid-19 na kuongeza idadi jumla ya maambukizi hayo nchini hadi 90,978.

Kwenye taarifa,waziri wa afya  Mutahi Kagwe alithibitisha kuwa idadi hiyo ilinakiliwa baada ya kupimwa kwa sampuli 8,230.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini sasa imetimia  960,364.

Idadi ya waliofariki nchini pia imeongezeka hadi 1,582 baada ya wahasiriwa wengine 14 kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Kagwe aliongeza kuwa wagonjwa 992 wamelazwa kwenye hosptali tofauti nchini.

Wengine 7,887 wanashughulikiwa wakiwa nyumbani.

Takriban wagonjwa 45 wamelazwa katika nyumba vya wagonjwa mahututi.

Wakati huo huo wagonjwa 325 wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kuongeza idadi ya waliopona ugonjwa huo nchini kutimia 71,579.

Kati ya walionakiliwa kuwa na ugonjwa huo 397 ni wakenya ilhali 276 ni raia wa kigeni.

Watu 397 walikuwa wa kiume ilhali wakike walikuwa 276 huku aliyekuwa na umri mdogo akiwa na miezi mitano na yule aliye na umri wa juu akiwa na miaka 86.

Nairobi iliongoza na maambukizi 211, Nakuru 113, Kilifi 61, Busia 41, Migori 34, Bungoma 33, Mombasa 32, Kiambu 21, Kakamega na Nyeri maambukizi 17 kila moja , Nyamira 15, Meru na Kirinyaga maambukizi 12 kila moja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *