Kenya yanakili visa 521 vipya vya Covid-19 huku watu 14 zaidi wakifariki

Kenya  imerekodi visa 521 zaidi vya maambukizi ya ugonjwa wa  Covid-19 katika kipindi cha saa 24  zilizopita na kufikisha 89,100 idadi ya jumla ya maambukizi ya ugonjwa huo.  

Kwenye hotuba kuhusu ugonjwa huo wa Covid-19 , katibu mwandamizi  Dkt. Mercy Mwangangi ametangaza kwamba sambuli 4,721 zilifanyiwa uchunguzi wakati wa kipindi hicho.

Kati ya visa hivyo, 315 ni wanaumme huku 206 wakiwa wanawake. Mdogo zaidi ni mtoto wa miaka mitatu huku mkongwe zaidi akiwa wa umri wa  miaka  tisini.

Amesema wagonjwa 14  wamefariki kutokana  na ugonjwa huo na kufikisha 1,545 idadi  ya jumla ya watu walioangamia kutokana na ugonjwa huo.

Wakati huo huo, wagonjwa  425 wamepata nafuu,  ambapo 330 kati yao ikiwa ni wale wanaaopewa huduma za matibabu Nyumbani, 95 kwenye hospitali mbali mbali  na kufikisha 69,839 idadi ya wagonjwa waliopona.

Katibu huyo mwandamizi amesema wagonjwa 1,102 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini na wengine 8,016 wakihudumiwa Nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *