Kenya yanakili visa 181 vipya vya Covid-19

Taifa hili limenakili visa 181 vipya vya Covid-19 baada ya kuchunguzwa kwa sampuli 5,577 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya maambukizi ya covid-19 hapa nchini sasa ni 105,648.

Kati ya visa hivyo vipya, 159 ni raia wa kenya huku 22 wakiwa raia wa kigeni. Mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa miezi miwili na yule mkongwe zaidi ana umri wa miaka 86.

Kaunti ya Nairobi iliongoza kwa Idadi ya visa vipya huku ikinakili visa104. Kaunti ya Kiambu ilikuwa ya pili kwa visa 20 huku Busia ikinakili visa 11.Nakuru iliandikisha visa 9.

Wakati huo huo wagonjwa wengine 88 wamepona virusi vya Covid-19 hapa nchini katika muda wa saa 24 zilizopita.

Wagonjwa 42 walikuwa katika mpango wa utunzi wa nyumbani na 46 waliruhusiwa kuondoka katika hospitali mbali mbali humu nchini.

Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni watu 86,609.

Hata hivyo Kulingana na taarifa ya wizara ya afya, mgonjwa mmoja zaidi amefariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya maafa kutokana na Covid-19 hapa nchini sasa ni 1,854.

Kwa sasa wagonjwa 347 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini huku wagonjwa 1,430 wakiuguzwa nyumbani.

Kwa mujibu wa wizara ya afya, wagonjwa 59 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo 25 Kati yao wanatumia vipumulio na 29 wanapokea hewa ya ziada ya oxygen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *