Kenya yalambishwa sakafu na Sudan Kusini CECAFA

Sudan Kusini imeibwaga Kenya  magoli 2-1 na kutwaa nishani ya shaba katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne ,ya michuano  ya Cecafa mwaka huu katika uwanja wa Black Rhino Academy huko Karatu mjini  Arusha Tanzania.

Philip Biajo aliiweka Sudan Kusini uongozini katika dakika ya 2  akiunganisha mpira uliotemwa na kipa wa Kenya.

Nicholas Ochieng aliisawazishia Kenya Risinga Stars katika dakika  ya 10 ya mchezo ,lakini Nelson Elija akifunga bao la uongozi tena kwa njia ya tikitaka na ushindi huo ukadumu hadi kipinga cha mwisho.

 

Matokeo ya mwaka huu yalikuwa mabovu kwa Kenya iliyopoteza katika fainali ya mwaka jana dhidi ya Tanzania nchini Uganda huku pia wakikosa kufuzu kwa makala ya 15 ya fainali za Afcon mwaka ujao nchini Mauritania.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *