Categories
Michezo

Kenya yaibwaga Ethiopia Cecafa

Rising Stars ya Kenya imeanza vyema mashindano ya kombe la Cecafa kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 baada ya kuilemea Ethiopia mabao 3 -0 katika mchuano wa kundi C uliosakatwa Jumatatu adhuhuri katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha .

Benson Omala licha kutemwa katika kikosi cha Harambee Stars alidhihirisha umahiri wake alilipopachika bao la dakika ya 37  kupitia kwa kichwa huku vijana wa Kenya wakienda mapumziko  kidedea kwa  bao hilo moja.

Kenya wakipiga dhidi ya Ethiopia uwanjani Sheikh Amri Abeid

Ronald Reagan aliongeza bao la pili mwanzoni mwa kipindi cha pili akitumia fursa ya makosa ya kipa wa Ethiopia huku  Enock Wanyama  akihitimisha karamu ya mabao ya wakenya.

Kenya watarejea uwanjani Ijumaa  hii kwa mchuano wa pili na wa mwisho  dhidi ya Sudan .

Timu mbili bora kutoka  kundi hilo zitafuzu kwa  hatua ya nusu fainali.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *