Kenya yaanza mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya CECAFA

Timu ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu kama  The Rising Stars, imeanza mazoezi Jumapili kujiandaa kwa mashindano yajayo ya Cecafa .

Kulingana na kocha wa timu hiyo Stanley Okumbi jumla ya wachezaji 27 walioripoti kambini Jumamosi walipimwa dhidi ya Covid 19 kuanzia mapema Jumapili  sawia na maafisa wa benchi ya kiufundi kabla ya kaunza mazoezi rasmi .

Kocha Okumbi anajivunia kuwa na vijana wengi walio na talanta huku akisema kuwa bado kuna pengo katika nafasi kadhaa katika timu ambazo atazijaza kabla ya kuelekea Tanzania  kwa mashindano hayo ya mwezi Ujao.

“Ninao vijana wengi walio na talanta katika timu ,kuna baadhi ya sehemu ambazo nitazijaza  ili tuwe na kikosi dhabiti  kwa mashindano hayo .Natarajia kuwaongeza wachezaji wachache timuni’’ akasema Okumbi

The Rising Stars wamo kundi  C  katika kipute cha mwaka huu pamoja na  Ethiopia na  Sudan.

Kwa mjibu wa kocha Okumbi timu hiyo itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sudan Jumatatu ya Novemba mbili na 5  katika uwanja wa taifa wa Nyayo kabla ya kusafiri kwenda Arusha.

Wachezaji wa The Rising Stars wakiwa mazoezini

Timu mbili bora kwenye mashindano hayo ya mjini Arusha Tanzania  baina ya Novemba 22 na Desemba 6 zitafuzu kuwakilisha ukandi huu katima mashindano ya Afcon mwaka ujao.

Tanzania maarufu kama Serengetio Boys ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kuilaza Kenya baoa 1-0  katika fainali  ya mwaka jana nchini Uganda .

Kikosi cha Rising Stars kilicho kambini kinawajumuisha:-

Makipa

Maxwell Mulili (AFC Leopards), Bixente Otieno ( Wazito), Elvis Ochieng (City Stars)

Mabeki

Boniface Mwangemi (Kariobangi Sharks), Omar Somobwana (AFC Leopards), Joseph Levin (Naivas), Wardfine Akhatsika (Chebuyusi High School), Kelvin Mose (Uweza), Alphonse Omija (Gor Mahia), Frank Odhiambo (Gor Mahia), Lewis Bandi (AFC Leopards), Fredrick Alushula (Kariobangi Sharks), Rolland Ashimoto (Wazito), Steiner Musasia (Talanta), Nicholas Omondi (Gor Mahia), Keith Imbali (Gor Mahia Youth)

Viungo

Enoch Wanyama (Ligi Ndogo), Ronald Reagan (Kariobangi Sharks), Alphonse Washe (Bandari), Hamid Mohammed (Bandari), Danson Kiprono (Zoo), Ian Simiyu (Nzoia Sugar), Austine Odhiambo (AFC Leopards), Mwakio Kisaka (Riruta United), Timothy Ouma (Nairobi City Stars), Telvin Maina (Kisumu All-Stars), Arnold Onyango (USA)

Washambulizi

Benson Omala (Gor Mahia), Henry Meja (Tusker), Stephen Otieno (Bongonaya), Kappen Samuel (Liberty), Sellasie Otieno (Liberty), Unaiz Shajani (Starfield Elite FC)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *