Kenya yaadhimisha siku 100 , kuanza kwa michezo Olimpiki ya Tokyo

Kenya imejiunga na ulimwengu Jumatano kusherehekea siku 100 kabla ya kuanza rasmi kwa makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan.

Waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed, aliwaongoza maafisa wa Nock katika uzinduzi wa hafla hiyo kwenye makao makuu ya makavazi ya kitaifa .

Waziri Amina amezindua kaulimbiu ya michezo ya mwaka huu ambayo itakuwa#YouAreTheReason kumaanisha ‘wewendiosababu‘ pamoja na tovuti rasmi ya michezo hiyo inayopatikana kupitia  teamkenya.or.ke.

Kenya itakuwa ikishiriki Olimpiki ya mwaka huu kwa mara ya 15  tangu mwaka 1954.

Michezo ya Olimpiki itaanza Julai 23 kwa sherehe ya ufunguzi   na kukamilika Agosti 8 mwaka huu baada ya kuahirishwa kutoka mwaka uliopita kutokana na janga la Covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *