Kenya U 17 yaning’inia Rwanda michuano ya CECAFA
Chipukizi wa Kenya walio chini ya umri wa miaka 17 wanahitaji maombi mengi na muujiza Ijumaa ili kufuzu kwa nusu fainali ya michuano ya CECAFA inayoendelea nchini Rwanda.
Kenya inayofunzwa na kocha Oliver Page itafuatilia kwa karibu pambano baina ya Ethiopia na mabingwa watetezi Uganda ambapo ili Kenya kufuzu kwa nusfu fainali ni sharti Uganda iwaadhibu Ethiopia mabao 6-0,baada ya Kenya kuchakazwa mabao 5-0 na Uganda katika mechi ya kundi A mapema wiki hii.
Uganda inaongoza kundi A kwa pointi 3 wakifuatwa na Ethiopia kwa alama 1 sawa Kenya waliokamilisha mechi zao hususan kufuatia kusajili sare ya 2-2 dhidi ya Ethiopia katika pambano la ufunguzi.
Timu mbili bora kutoka kundi hilo zitafuzu kupiga nusu fainali dhidi ya timu mbili bora kutoka kundi B .
Timu ya kwanza na ya pili zitafuzu kushiriki fainali za AFCON mwaka ujao nchini Moroko.