Kenya kupambana na Uganda nusu fainali ya CECAFA Jumatatu
Chipukizi wa Kenya walio chini ya umri wa miaka 20 watashuka uwanjani Black Rhino Academy sports Complex Jumatatu Novemba 30 kuanzia saa sita adhuhuri kupambana na majirani Uganda katika nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la Cecafa mjini Arusha Tanzania.
Kenya ijulikanayo kama Rising Stars iliongoaza kundi C kwa alama 6 baada ya kuwalemea Ethiopia mabao 3-0 katika mechi ya kwanza kabla ya kuilaza Sudan mabao 2-1 katika mechi ya mwisho .
KENYA RISING STARS
Kwa upande wao Uganda waliongoza pia kundi B kwa pointi 4 baada ya kwenda sara tasa dhidi ya Sudan Kusini, kabla ya kuiparamia Burundi mabao 6-1 katika mechi ya mwisho .
Nusu fainali ya mwisho itang’oa nanga mida ya saa tisa unusu katika uwanja uo huo kati ya mabingwa watetezi na wenyeji Tanzania dhidi ya Sudan Kuisini.
UGANDA HIPPOS
Tanzania maarufu kama Ngorongoro Heroes walianza kwa ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Djibouti katika mechi ya ufunguzi ya kundi A ,kabla ya kuisasambua Somalia mabao 8-1 katika mechi ya pili na kuongoza kundi kwa alama 6.
TANZANIA NGORONGORO HEROES
Sudan Kusini nao waliibuka wa pili kundi B kwa alama 4 wakienda sare kapa dhidi ya Uganda na kuipiku Burundi magoli 4-0 katika mechi ya mwisho.
Washindi wa nusu fainali za Jumatatu watafuzu kushiriki mashindano ya kombe la Afcon mwaka ujao nchini Mauritania pamoja na kumenyana kwenye fainali ya Disemba 2 kubaini mabingwa.
SOUTH SUDAN
Tanzania walitwaa kombe hilo mwaka jana nchini Uganda baad ya kuipiga Kenya fainalini.