Categories
Michezo

Kenya kukabana koo na Ethiopia Jumatatu katika michuano ya CECAFA

Timu ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 itaanza harakati za kuwania kombe la Cecafa katika kundi C dhidi ya Ethiopia Jumatatu adhuhuri katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  mjini Arusha Tanzania.

Rising Stars inayofunzwa na kocha Stanley Okumbi italenga kuboresha matokeo ya mwaka jana waliposhindwa kwenye fainali  bao 1 kwa bila na Ngorongoro Heroes ya  Tanzania .

Kenya U 20 wakimiliki Mpira dhidi a Sudan Uwanjani Nyayo        picha  @Mnyamwezi

Kando na kombe la Cecafa,mashindano hayo yatakayokamilika tarehe 2 mwezi ujao pia yatatumika kuteua timu mbili bora zitakazowakilisha ukanda wa Cecafa katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon kwa vijjana walio chini ya umri wa miaka 20 yatakayoandaliwa nchini Mauritania baina ya Januari na Februari mwakani.

Baada ya pambano la leo Kenya watarejea uwanjani Ijumaa hii kwa mechi ya mwisho dhidi ya Sudan kabla ya mapambano ya nusu fainali kuchezwa Novemba 30.

Mashindano ya Cecafa yanayoshiriksiha mataifa 9  yalianza jana mjini Arusha huku wenyeji na mabingwa watetezi Tanzania wakiititiga Djibouti mabao 6-1 na yataingia siku ya pili leo kwa jumla ya mechi mbili.

Tanzania wakichuana na Djibouti katika mchuano wa ufunguzi Jumapili

Uganda na Sudan kusini watamaliza udhia uwanjani Sheikh Amri Abeid saa kumi alasiri katika mechi ya kwanza ya kundi B ,baada ya Kenya na Ethiopia kufungua pazia la kundi C katika uga uo huo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *