Kenya kuimarisha uzalishaji samaki katika kaunti 15

Taifa hili linalenga kuimarisha  uzalishaji wa samaki kutoka kiwango cha tani elfu tatu hadi zaidi ya tani laki moja katika muda wa mwaka mmoja ujao.

Haya yanafuatia msaada wa pesa wa shilingi bilioni 15 kutoka hazina ya ustawi wa kilimo ambayo inalenga kuimarisha biashara ya kuvua samaki katika kaunti  15.

Katibu katika idara ya uvuvi na maswala ya uchumi wa baharini Prof Micheni Ntiba ambaye alikuwa akiongea huko  Kisumu alisema kuvua samaki katika mfumo wa kiasili wa maji kunaendelea kukabiliwa na utata.

Prof. Ntiba alisema kuwa kwa sasa serikali inalenga kuwahimiza wavuvi wa samaki kujiunga na kilimo cha ufugaji wa samaki ili kubuni nafasi za ajira, kuimarisha uwepo wa chakula na kuimarisha mahitaji ya lishe bora.

Alisema kuwa serikali inabuni eneo la kisasa la kukuza  samaki ili kuimarisha uzalishaji wa samaki.

Katibu huyo alisema kuwa shirika la IFAD linafadhili mradi huo kupitia kwa mpango wa kukuza biashara ya samaki katika kaunti 15 na maeneo 180 kote nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *