Kenya kuandaa mashindano ya kufana ya Kip Keino classic Asema Tuwei

Rais wa chama cha riadha Kenya jen mstaafu Jackson Tuwei ana imani kuwa Kenya itaandaa mashindano ya kufana ya Kip Keino Classic jumamosi hii katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Yatakuwa mashindano ya kwanza Afrika mwaka huu huku zaidi ya wanariadha 150 wa humu nchini wakitarajiwa kushiriki.
Mashindano ya jumamosi yatakuwa ya vitengo vita vitatu huku wanariadha wengi mashuhuri wa humu nchini wakitarajiwa kushiriki .

Pia mashabiki wasiozidi 10,000 wanatarajiwa kushiriki.

Kulingana na Tuwei Kenya ina uwezo wa kuandaa mashindano ya riadha ulimwenguni mwaka 2025 kwani miundo msingi imeboreshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *