Kenya inakabiliwa na upungufu wa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi

Chama cha wamiliki wa duka za kuuza dawa humu nchini -PSK, kimetoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati haraka ili kuepusha mgogoro unao-nukia kuhusu dawa za kupunguza makali ya ukimwi.

Kwenye taarifa kwa vyumba vya habari, Rais wa chama hicho Dkt. Louis Machogu, alidai kwamba uhaba mkubwa wa dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARVs), unanukia humu nchini kufuatia mzozo baina ya serikali ya Kenya na shirika la USAID.

Alisema kwamba Rais Kenyatta anapaswa kuziagiza mara moja wizara za mashauri ya nchi za kigeni, afya, na fedha kusuluhisha mzozo ulioko wa kibalozi kuepusha mgogoro mkubwa.

Aidha,Machogu alishauri wahusika wa mipango yote ya utoaji misaada, kuhakikisha kwamba wataalamu wao wa mipango ya usambazaji na pia ma-meneja wa miradi, wamejifahamisha na taratibu na pia idhini zinazohitajika, ili kulainisha shughuli hizo na kuokoa muda.

Alitoa wito kwa taasisi zinazohusika na uagizaji serikalini, kulainisha mipango yao ili kurahisisha ushirikiano wa wawekezaji na pia wafadhili na serikali katika utoaji dawa kwa wote.

Wakati huo huo; Machogu alihimiza baraza la ma-waziri kushughulikia haraka vifaa vya kujikinga ambavyo bado vinazuiliwa na shirika la usambazaji vifaa vya matibabu -(KEMSA), ili vipelekwe kwenye taasisi za afya za umma kwa bei ya sasa na kutumiwa kabla ya muda wa matumizi yake kutamatika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *