Kenya Cup Kung’oa nanga Jumamosi kwa mechi 4

Mashindano ya kuwania kombe la Kenya Cup yataanza rasmi Februari 27 kwa mechi 4 baada ya mapumziko marefu yaliyosababishwa na janga la Covid 19.

Michuano miwili ya mkondo wa kwanza itaandaliwa katika uwanja wa kilabu cha Nakuru Athletic , Menengai Oilers wakipambana na Kenya Harlequin katika mechi ya ufunguzi kabla ya Top Fry Nakuru kupimana ubabe na Blak Blad.

KCB wakiwa mazoezini

Mabingwa watetezi KCB watakuwa nyumbani Ruaraka dhidi ya Strathmore Leos iliyopandishwa daraja msimu huu wakati Kabras Sugar ikiwaalika Masinde Muliro katika derby ya Kakamega maarufu kama Katch Derby katika uwanja wa Moi Kakamega Showground.

Mashindano ya kenya Cup hushirikisha timu za wachezaji 15 kila upande na huwa na ushindani na ufuasi mkubwa nchini .

Mashindano hayo yalianzishwa mwaka 2014 Nakuru Rfc wakitawazwa mabingwa msimu wa mwaka 2014/2015 nao Impala Saraceans wakinyakua taji ya simu wa mwaka 2015/2016 kabla ya kuwapisha Homeboyz mwaka 2016/2017 nao KCB wakalishinda mwaka 2017/2018 huku Kabrasa wakishinda msimu wa 2018/2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *