KEBS yaidhinisha mwongozo wa utayarishaji wadudu wanaoliwa

Ajenda nne kuu za serikali kuhusu uwepo wa chakula cha kutosha ilipigwa jeki baada ya shirika la kukadiria ubora wa bidhaa-KEBS kuidhinisha viwango vitatu ambavyo vitatoa mwongozo wa utayarishaji wa kimsingi wa wadudu wanaoliwa na bidhaa zinazotokana na wadudu hao.

Miongozo hiyo inawadia huku shinikizo kuhusiana na vyanzo vya jadi vya madini ya  proteini, carbohydrates na mafuta vikizidi kudidimia.

Hali hii imesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya vyakula mbadala vya kufidia hali hiyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la KEBS  Luteni kanali mstaafu Bernard Njiraini, viwango hivyo ambavyo ndivyo vya kwanza kuchapishwa kama viwango vya kwanza vya kitaifa ulimwenguni, vinatarajiwa kusaidia ubunifu unaoendelea hasa katika utengenezaji wa bidhaa na kuboresha thamani ya bidhaa za Kenya kimataifa huku mahitaji ya kimataifa ya wadudu wanaoliwa yakizidi kuongezeka.

Hatua hii ya shirika la  KEBS itaimarisha aina za lishe na kupunguza shinikizo kwenye vyakula vya kawaida na kufanikisha ajenda nne kuu za serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *