KBC Channel One kuonyesha mechi ya Kenya dhidi ya Comoros Jumatano

Runinga ya taifa KBC itapeperusha mbashara mchuano wa kundi G kufuzu kwa dimba la Afcon Jumatano hii baina ya Harambee Stars dhidi ya wageni Comoros kuanzia saa moja usiku kutoka uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

KBC Channel one imeshirikiana na  kampuni ya Betika kuhakisha mashabiki wanapata mechi hiyo moja kwa moja baada ya mashabiki kuzuiwa kuingia uwanjani kutokana na ugonjwa wa Covid 19.

Harambee Stars hawana budi kushinda mchuano huo ili kuwa na matumaini ya kufuzu kwenda Cameroon Juni mwaka ujao kwa kipute cha Afcon .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *