KBC channel 1 kupeperusha Nusu fainali za mataji ya CAF baina ya vilabu

Wapenzi wa soka nchini watapata fursa ya kushuhudia mbashara  nusu fainali  za ligi ya barani Afrika na .

Runinga ya KBC imekuwa ikipeperusha mechi za ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho la kandanda Afrika tangu msimu ulipoanza,huku mechi hizo zikisitishwa kwa takrina miezi sita kutokana na janga la covid 19.

Nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika itapigwa Jumamosi hii Wydad Casablanca ya Moroko ikiwaalika mabingwa mara nane Al Alhy ya Misri katika uwanja wa Mohammed V  kuanzia saa nne usiku majira ya Afrika mashariki.

Al Ahly

Wenyeji Wydad watakuwa wakicheza nusu fainali kwa mara ya sita  huku wakitinga fainali mara 4,ingawa wanajivunia rekodi nzuri ya nyumbani ambapo wamepoteza mechi 2 kati ya 10 walizocheza ,kushinda 5 na kutoka sare mara tatu.

Pia Wydad hawajapoteza katika mechi 26 za nyumbani katika ligi ya mabingwa na sadfa kubwa kipigo cha mwisho nyumbani kilikuwa dhidi ya Al Ahly Julai 27 mwaka 2016.

Al Ahly maarufu kama Red Devils watakuwa wakicheza nusu fainali kwa mara ya 16 wakifuzu fainali mara 12 na kutawazwa mabingwa mara nane. They have progressed 12 times.

Al Ahly wamepoteza mechi mbili wakiwazuru  Wydad na wamefunga bao katika mechi zao nne za mwisho ugenini katika kombe hili.

 

Wydad Casablanca

Jumapili itakuwa zamu ya  Raja Casablanca pia ya Moroko kuwakabili  Zamalek kutoka Misri pia mida ya saa nne usiku.

Raja watakutana na Zamalek kwa ya tatu Jumapili huku wakitafuta ushindi wa kwanza dhidi ya wageni,baada ya Zamalek kushinda mechi moja na nyingine kuishia sare.

Raja watakuwa wakipiga nusu fainali ya ligi ya mabingwa kwa mara ya 6 wakifuzu kwa fainali mara nne na kwa jumla wamepoteza mechi moja pekee nyumban katika mechi 22.

Raja Casablanca

Zamalek nao watakuwa nusu fainali kwa mara ya 10 wakitinga fainali mara 7 na wamepoteza mechi mbili pekee katika mechi 9 za ligi ya mabingwa.

Hata hivyo Zamalek wana rekodi mbovu ugenini wakishinda mchuano mmoja kati ya 13 za ugenini katika kombe hilo.

 

Zamalek

Nusu fainali za kombe la shirikisho zitachezwa kwa mkunmbo mmoja ,Rs Berkane ya Moroko ikimenyana na wenzao Hassani Agadir  tarehe 19 huku Pyramids kutoka Misri ikiwaalika Horoya Ac kutoka Guinea tarehe 20.

Fainali ya kombe hilo itasakatwa 25 mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *