KBC Channel 1 kupeperusha mbashara Fiba Afrobasket

Runinga ya Taifa KBC Channel 1 itapeperusha mechi za makundi za timu ya Taifa ya mpira wa kikapu kwa wanaume al-maarufu Morans kwenye mashindano ya kufuzu kwa michuano ya FIBA Afro Basket mwakani mjini Kigali Rwanda kati ya Novemba 25 na 29 mwaka huu.

Kenya ilishiriki mashindano hayo mara ya mwisho mwaka 1993 jijini Nairobi ikiwa mwenyeji na inalenga kufuzu kwa mara ya pili baada ya kuyakosa kwa takriban mwongo mmoja.

Hata hivyo, ili ifuzu ni sharti imalize miongoni mwa timu tatu bora kutoka kundi B linaloshirikisha Angola, Senegal na Msumbiji.

Morans  watafungua  ratiba ya kundi B dhidi ya Senegal Jumatano hii kuanzia saa kumi na mbili jioni kabla  kurejea uwanjani Kigali Alhamisi  dhidi ya miamba Angola kuanzia saa tisa  na kufunga ratiba dhidi ya Msumbiji Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili jioni.

Timu 20 zinashiriki mashindano hayo huku mataifa matatu bora kutoka kila kundi yakifuzu kwa mashindano ya Fiba Afrobasket mwaka  ujao  .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *