Kazi ya kwanza ya Prince Harry na Meghan Markle ambayo itaonyeshwa kwenye Netflix

Meghan Markle na mume wake Prince Harry wametangaza kazi yao ya kwanza chini ya kampuni yao ya kuunda filamu kwa jina “Archewell Productions”.

Filamu yao ya kwanza kwa jina “Heart of Invictus” ni ya matukio halisi na wahusika halisi na itaangazia kazi yao ya msaada ambayo inafahamika kama “The Invictus Games”.

Mwaka 2014, Prince Harry alianzisha mpango huo wa msaada kwa wanajeshi ambao wamejeruhiwa na waliostaafu ambao unahusu mashindano ya michezo kati yao.

Usimamizi wa The Invictus Games ndio ulitangaza Jumanne kwamba Archewell Productions itawaangazia kwenye filamu ya matukio halisi ambayo baadaye itapatikana kwenye jukwaa la Netflix.

Safari za wanamichezo binafsi wanaoshiriki mashindano hayo zitaangaziwa huku awamu nyingine ya mashindano ikipangiwa kufanyika mwaka 2022 mjini The Hague, huko Netherlands.

Prince Harry anasema tangu aanzishe mashindano hayo, alijua kwamba kila mshindani angechangia picha ya kutokata tamaa, ari na kujitolea maishani na sasa filamu hiyo itatoa nafasi kwa ulimwengu kufahamu historia ya washindani hao hata wanapojiandaa kwenda Netherlands.

Harry ni mmoja wa watayarishi wakuu lakini ataangaziwa pia kwa kazi hiyo itakayoelekezwa na Orlando von Einsiedel wa uingereza na kutayarishwa na Joanna Natasegara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *