‘Kazi ipo ‘asema kocha mpya wa Gor Mahia Roberto Oliveira baada ya kushika hatamu

Kocha mya wa mabingwa wa ligi kuu Gor Mahia Roberto Oliveira amesema ana kibarua kigumu katika majukumu yake mapya ya kuwanoa Kogalo.

Oliveira ambaye ni raia wa Brazil alisema haya punde baada ya kutambulishwa katika timu ya Gor ,akiongeza kuwa atakuwa na kibarua cha ziada timuni kutokana na rekodi nzuri ya timu hiyo iliyoshinda ubingwa wa ligi mara 18.

Kocha huyo ana tajriba ya ukufunzi ya miaka 25 barani Afrika,Mashariki ya kati na nyumbani Brazil.

Oliveira anasema amekuwa akimezea mate kazi hiyo na komba ushirikiano kutoka kwa maafisa wengine wa benchi ya kiufundi na wachezaji ili kuafikia ufani.

Baada ya kuigura Rayon sports ,nilipata ofa tatu za kurejea kufunza Afrika lakini nikadinda lakini singekataa ofa ya  Gor mahia kutokana na mbinu yao ya uchezaji.nimefurahia fursa hii’’akasema kocha Roberto

Roberto anatwaa ukufunzi wa Kogalo kutoka kwa  Steven Polack aliyejiuzulu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *