Kaunti zilizopakana na Ziwa Victoria kukumbwa na mafuriko

Kaunti za Busia, Siaya, Homa Bay na Migori zimo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na mafuriko kutokana na ongezeko la kiwango cha maji kwenye Ziwa Viktoria.

Mamia ya familia zimelazimika kuhama makwao huku mali ikiharibiwa kufuatia mafuriko katika eneo la Budalangi.

Tume inayoshughulikia eneo la Ziwa Viktoria chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeweka mikakati ya kuisaidia Kaunti ya Siaya kukabiliana na changamoto hizo.

Haya yalisemwa wakati wa mkutano ulioandaliwa Mjini Naivasha kati ya maafisa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wale wa serikali ya kaunti.

Kwa mujibu wa Mayani Saino kutoka Wizara ya Mazingira, athari za mabadiliko ya hali ya anga zinadhihirika pakubwa katika kaunti hizo.

Kwa upande wake katibu mkuu wa tume ya eneo la Ziwa Viktoria, Dkt. Ali Matano alisema changamoto kuu kwa sasa ni ongezeko la kiwango cha maji cha Ziwa Viktoria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *