Categories
Michezo

Katibu mkuu wa FKF Barry Otieno apigwa marufuku ya miezi 6 na CAF kwa utundu

Sherikisho la kandanda barani Afrika Caf limempiga marufuku ya miezi 6 katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF Barry Otieno kwa utundu na ukaidi wakati wa mechi ya marudio ya kundi F kufuzu kwa fainali za AFCON dhidi ya Comoros mjini Moroni mwezi Novemba mwaka jana ambapo Kenya ilishindwa mabao 1-2.

Imebainika kuwa Otieno wakiwa na Team Manager wa Kenya Ronny Oyando walichelewesha na kukataa kutoa matokeo ya uchunguzi wa COVID 19 maarufu kama PCR tests ya wachezaji  wa Harambee Stars na kuchelewesha matokeo hayo kwa takriban saa tatu na kuyatoa muda mchache kabla ya kuanza kwa mechi.

Kamisaa wa mechi hiyo hakupata fursa ya kuangalia matokeo hayo baada ya Otieno na Oyando kumpokonya karatasi hiyo na kuirarua wakipinga matokeo ambapo wachezaji wane  wa Harambee Stars walikuwa wamepatikana na  COVID 19.

Uchunguzi wa matokeo hayo baada ya mechi uliashiria Kenya ilichezesha wachezaji 4 waliokuwa na virusi vya korona hivyo kuhatarisha maisha ya wachezaji na maafisa wengine waliokuwa katika mechi hiyo na kukiuka sheria za CAF kuhusu COVID 19.

Kufuatia kosa hilo FKF imepigwa faini ya shilingi milioni 2  huku Barry Otieno na Ronny Oyando wakifungiwa kujihusisha na mechi wala mashindano yoyote ya CAF kwa kipindi cha miezi 6.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *