Kate Actress amefiwa

Muigizaji Catherene Kamau maarufu kama Kate Actress amefiwa na shemeji yake mume wa dadake. Alitangaza hayo kupitia mitandao ya kijamii huku akiomba wafuasi na mashabiki waikumbuke familia hiyo katika maombi.

Kwenye akaunti yake ya Instagram, Kate aliweka picha ya dadake, mume wake na mtoto wao na kuandika, “Mpwa wangu amepoteza babake, dadangu amepoteza rafiki yake wa dhati. Jamani kifo kamwe hakikutayarishi! Brian nina heshima kubwa sana kwako, ulimpenda binti yako sana, dadangu Nyambu amechanganyikiwa. Najaribu kukubali kwamba hauko tena. Mama amepoteza mtoto wake, familia yako ina majonzi mengi uliondoka mapema. Lala salama baba Bunbun (Samara). lala salama Brian Safari. Mtukumbuke kwa maombi.”

Watu wengi maarufu nchini Kenya walimwandikia maneno ya kumtia moyo Kate Actress kama vile muigizaji Milly Chebby mke wa Terrance Creative aliyeandika, “I am so sorry for your loss hun may God give your family peace that passes all human understanding.”

Kalekye Mumo ambaye alikuwa mtangazaji wa redio alimwambia, “My deepest condolences to you and the whole family. May his soul Rest In Peace”.

Kate Actress ambaye ni mke wa mtayarishaji wa vipindi Philip Karanja, baadaye tena aliweka picha ya marehemu shemeji yake na kuongeza maneno, “Fare thee well bro. Greatest Dad ever.”

Tunaitakia familia nzima faraja wakati huu wa majonzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *