Categories
Burudani

Kanye West atoa viatu vyake kwa nyumba ya Kim Kardashian

Mwanamuziki wa Marekani Kanye West na mwanamitindo Kim Kardashian wanaendelea kuchukua hatua ambazo zinathibitisha taarifa kuhusu ndoa yao kufika mwisho.

Hatua ya hivi karibuni aliyochukua Kanye West ni kuondoa jozi zipatazo 500 za viatu vyake kutoka kwa nyumba ya Calabasas ambayo Kim Kardashian anakaa na watoto wao watano.
Kanye kwa sasa anaishi kwenye nyumba yao nyingine katika eneo la Wyoming na kwamba yeye na Kim hawaongei kabisa.

Ripoti zinaonyesha kwamba Kanye pia alipanga vitu vyake vingine vikatolewa kwenye nyumba hiyo ya Kim na watoto wao.
Jambo lingine ambalo lilisababisha minong’ono kuhusu kuvunjika kwa ndoa ya Kanye na Kim, ni hatua yao ya kuacha kuhudhuria vikao vya ushauri wa ndoa.

Mwezi Julai mwaka 2020, ripoti zilionyesha kwamba Kim alikuwa ametafuta wakili tayari kuanza mipango ya talaka kortini.

Inasemekana kwamba mipango ishakamilika ya Kim kuanzisha kesi ya talaka na anasubiria wakati mwafaka.

Kim Kardashian na Kanye West walifunga ndoa mwaka 2014 nchini Italia na miaka michache baadaye kitumbua kimeingia mchanga.

Wanandoa hao wawili walikuwa wakikosana ilivyo kawaida kwenye ndoa lakini kilichomkera Kim Kardashian kabisa ni hatua ya Kanye ya kuwania urais nchini Marekani.

Kulingana naye hilo halikuwa jambo ambalo walijadiliana na kupanga ila Kanye alikurupuka tu na kuanza kampeni za kuwania urais.

Kanye huwa na tatizo la msongo wa mawazo ambalo husababisha mtu afanye mambo bila kutathmini na wakati mmoja anaonekana mwenye raha na wakati mwingine amehuzunika.

Mwanamuziki huyo alikuwa anaacha kutumia dawa inavyohitajika na hilo pia lilikasirisha mke wake Kim Kardashian.

Kipindi cha familia ya Kim almaarufu Keeping Up With The Kardashians kinaelekea kufika mwisho na inasemekana utengano wa Kim na Kanye huenda ukaangaziwa kwenye awamu ya mwisho ya kipindi hicho kwani kamera zimeonekana zikimwandama Kim ambaye sasa amejifunza kulea watoto wake peke yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *