Kanayo .O. Kanayo muigizaji maarufu nchini Nigeria sasa ni wakili aliyehitimu

Mwigizaji wa muda mrefu kwenye filamu za nchi ya Nigeria almaarufu Nollywood, Kanayo .O. Kanayo sasa ni wakili aliyehitimu kuhudumu nchini Nigeria.

 

Hii ni baada yake kupatiwa kibali rasmi cha kuhudumu chini ya mahakama ya juu nchini Nigeria kitu ambacho kwa lugha ya kimombo huitwa “admission to the bar”. 

 

Kanayo alitumia mtandao wa Intagram kutangaza habari hizo njema kwa wafuasi wake.

 

 

Anayo Modestus Onyekwere alizaliwa mwezi tarehe mosi machi mwaka 1962 eneo la Imo state nchini Nigeria. Ni wakili na muigizaji. Mwaka 2006 alishinda tuzo la muigizaji bora kwenye tuzo za African Movie Academy Award kwa jukumu lake kwenye filamu kwa jina “family battle”.

 

Alianza rasmi kuigiza mwaka 1992, ni balozi wa umoja wa mataifa au ukipenda United Nations na ni mmoja wa watu ambao walipata kutuzwa na serikali ya Nigeria mwaka 2014 wakati wa kusherehekea miaka 100.

 

Kanayo alijiunga na chuo kikuu cha Abuja na mwaka 2019 akafuzu na shahada ya uanasheria na baadaye akajiunga na shule ya uanasheria ya Nigeria bewa la Abuja. Mwaka huu amefuzu kuwa wakili kamili. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *