Kalekwa aitaka serikali kuruhusu kuanza kwa ligi kuu ya FKF

Rais wa kilabu ya Sofapaka Elly Kalekwa ameitaka wizara ya afya na ile ya michezo kuruhusu kurejea kwa  soka humu nchini ili ligi kuu ya FKF ianze ilivyoratibiwa tarehe 20 mwezi huu.

Akizungumza kwa njia kipee na KBC Kalekwa amesema kuwa ni wakati mwafaka wa kuanzisha ligi huku mchezo wa soka ukitoa ajira kwa vijana wengi humu nchini.

‘’sisi tuko tayari kuzingatia masharti yote ya Covid 19 ,kwa hivyo tunaiomba serikali iruhusu soka irejee’’akasema Kalekwa

Kalekwa ameongeza kuwa hali ya ugonjwa wa Covid 19 bado haitabiriki sawa na mataifa ya Ulaya ambayo tayari yamerejelea ligi zao ,ligi kuu inaweza kuchezwa bila mashabiki katika viwanja na kufuata itifaki zote za afya.’’ukiangalia ulaya wameendelea na ligi zao pia sisi tunanaweza kucheza bila mashabiki na  tufuate masharti yote ya afya’’akaongeza Kalekwa

Wachezaji wa Sofapaka wakiwa mazoezini katika uwanja wa shule ya Eastleigh High

Kinara huyo amefafanua kuwa wamekamilisha usajili wa wachezaji wapya na wako tayari kuanza msimu huku wakilenga kunyakua ubingwa wa ligi kuu.

‘’kwa saa hii tumemaliza kusajili wachezaji katika idara zilizokuwa na mapungufu na tuko tayari kwa msimu mpya tukilenga kushinda taji ya ligi kuu’’akasema kalekwa

Kalekwa aliyasema haya kihudhuria mazoezi ya timu hiyo katika shule ya upili ya Eastleigh .

Msimu mpya wa ligi kuu ya FKF umeratibiwa kuanza rasmi tarehe 20 mwezi huu na kukamilika Mei mwakani ingawa wizara ya Michezo bado haijatoa idhini kwa ligi hiyo kuanza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *