Kafyu ya usiku nchini Rwanda yapunguzwa kwa saa mbili

Baraza la mawaziri nchini Rwanda limepunguza kafyu ya usiku kwa muda wa saa mbili huku visa vya maambukizi ya virusi vya corona vikipungua.

Kafyu hiyo sasa itakuwa kati ya saa nne usiku na saa kumi alfajiri. Huduma ya uchukuzi wa umma utarejelewa kikamilifu kwa abiria wanaoketi huku wale wanaosimama wakiwa nusu ya idadi ya kawaida.

Aidha,watu wanaohudhuria mikutano ya kukongamana kwa sasa hawatahitajika kuwa na cheti ya kuonyesha hawajaambukizwa ugonjwa wa Covid 19.

Hata hivyo waandalizi watahitajika kufuata maagizo yakutokaribiana kwa kuhakikisha kwamba asilimia 50 ya idadi ya kawaida ya watu ndio wanahudhuria vikao hivyo.

Baraza la mawaziri lilisema faini inayotozwa kwa kukosa kuvalia barakoa pamoja na kutozingatia kafyu ya usiku itasalia vivyo hivyo.

Wale watakaopatikana bila maski kwenye maeneo ya umma watatozwa faini ya dola 10 za marekani.

Faini sawia na hiyo itatozwa kwa wale wasiozingatia umbali unaohitajika wa mita mbili baina ya watu au kupuuza kafyu ya usiku.

Kufikia sasa,Rwanda imethibitisha visa  4,905 vya virusi vya korona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *