Juliani kuhutubia mhadhiri na wanafunzi wa chuo Kimoja huko Canada

Mwanamuziki wa nchi ya Kenya Juliani ametangaza kwamba atakuwa na mazungumzo na mhadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha Carleton kilichoko nchini Canada.

Mazungumzo yenyewe yatahusu kitabu kwa jina “The Street Is My Pulpit: Hip Hop and Christianity in Kenya” ambacho kimeandikwa na mhadhiri wa Marekani wa asili ya Kenya Mwenda Ntarangwi.

Picha ya Juliani akiwa anaimba ndiyo iko kwenye jalada la kitabu hicho ambacho kilizinduliwa rasmi tarehe 4 mwezi Mei mwaka 2016.

Kwenye kitabu hicho, Mwenda ambaye anafundisha katika chuo kikuu cha Calvin huko Marekani, anasimulia jinsi muziki aina ya Hip Hop unahusiana na Ukristo nchini Kenya.

Julius Owino maarufu kama Juliani anasema amekuwa akifahamu kwamba maneno yana uwezo mkubwa katika kunakili mambo ya nyakati, kuhamasisha na kuunda uhalisia wa siku za usoni lakini Mwenda alipoandika kitabu hicho alimthibitishia hayo.

Juliani anayefahamika sana kwa kibao “Utawala” anasema sanaa na muziki vina nafasi katika jamii zaidi ya burudani tu.

Haya yanajiri wakati Juliani anapanga kuachilia albamu yake ya nne kwa jina Master Piece ambayo itapatikana kwenye majukwaa kadhaa ya mtandao.

Albamu hiyo itakuwa na vibao 12 ambavyo ni;

1. Snobbish Old man
2. Simultaneously
3. Blah Blah Blah
4. Many Dan Dem
5. Story za Tene
6. Just another Tuesday
7. C’EST La Vie
8. Inheritance ya Kamba
9. Mabawa
10.Tumbo 2 Tombstone
11.Locks to my Socks
12.Masters Piece

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *